s

Chanzo cha picha, Mwananchi

Leo, Mahakama Kuu Masjala ndogo ya Dar es Salaam imesoma shitaka linalomkabili Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani Tanzania, Chadema, Tundu Lissu, katika kesi ya uhaini. Lissu amesomewa shitaka hilo kwa mara ya kwanza Mahakama kuu mbele ya jopo la majaji na kukana.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 6, 2025, baada ya upande wa utetezi kutoa orodha ya mashahidi wake. Awali, Mahakama ilikuwa imetupilia mbali hoja zote za pingamizi la Lissu kuhusiana na uhalali wa hati ya mashtaka.

Lissu alihoji kuwa hati ya mashtaka haionyeshi maelezo ya kosa wala nia ya kutenda uhaini, vipengele ambavyo ni muhimu katika kesi ya aina hiyo.

Hata hivyo, Jaji Dunstan Ndunguru alieleza kuwa Mahakama imeridhika hati ya mashtaka ipo sahihi na inatoa maelezo ya kosa kama sheria inavyotaka. Suala la nia ya kutenda kosa hilo litaamuliwa kupitia ushahidi unaotarajiwa kuwasilishwa mahakamani.



Source link

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *