Julian Alvarez

Chanzo cha picha, Getty Images

Mshambuliaji wa zamani wa Manchester City Julian Alvarez, 25, anafikiria kuondoka Atletico Madrid msimu ujao, huku Liverpool na Barcelona zikiwa na nia ya kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina. (Fichajes – kwa Kihispania)

Wasiwasi wa West Ham kuhusu mahitaji ya kifedha ya Nuno Espirito Santo unaweza kutoa mwanya kwa Slaven Bilic kuchukua nafasi ya Graham Potter, ambaye anang’ang’ania kibarua chake baada ya mwanzo mbaya wa The Hammers msimu huu. (Guardian)

Barcelona inataka kufikia makubaliano na Manchester United ili kumsajili mshambuliaji wa Uingereza ambaye alijiunga na klabu hiyo kwa mkopo Marcus Rashford, 27, kwa £26m – ada ambayo haikidhi kiwango kinachotakiwa na United, ya takribani na £35m. (Star)

Real Madrid ilimfuatilia William Saliba, 24, katika mechi ya Arsenal dhidi ya Manchester City Jumapili, kuashiria kuwa bado ina nia ya kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa. (TBR Football)

Nahodha wa Crystal Palace na beki wa England Marc Guehi, 25, bado ana hamu ya kujiunga na Liverpool kama mchezaji huru msimu ujao, baada ya kukaribia kusajiliwa na mabingwa hao wa Ligi ya Premia siku ya mwisho ya uhamisho wa wachezaji. (GiveMeSport)

Tottenham bado ina nia ya kumsajili winga wa Manchester City Savinho, 21, na wanaweza kutathmini upya mpango wa kumsaini mshambuliaji huyo wa Brazil mwezi Januari. (Team talk)

Savinho

Chanzo cha picha, Getty Images

Spurs pia iko tayari kutoa hadi pauni milioni 35 kumsajili kiungo wa kati wa Real Sociedad na Uhispania Brais Mendez, 28, mwezi Januari. (Fichajes – kwa Kihispania)

Chelsea inamnyatia Nico O’Reilly Manchester City, huku Leeds United, Bayer Leverkusen na Lyon pia zikimuwania mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20. (Football Insider)

Manchester United imepatia kipaumbele “usajili wa kipa mkuu” msimu ujao wa kiangazi. (Sun)

Pia unaweza kusoma:

Imetafsiriwa na Ambia Hirsi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *