Nchi za Burkina Faso na Mali, zinazoongozwa na wanajeshi, hazikutuma wawakilishi kwenye mkutano wa wakuu wa majeshi barani Afrika unaofanyika kwa siku nchini Nigeria.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mkutano huo unaofanyika jijini Abuja, ulifunguliwa siku ya Jumatatu, wakati huu  uhusiano kati ya nchi hizo zilizounda umoja wao wa mataifa ya Sahel ukiendelea kuwa mbaya na jirani zake katika ukanda wa Afrika Magharibi.

Niger, ambayo pia inaongozwa na jeshi na ipo katika kundi moja na Burkina Faso na Mali, inawakilishwa kwenye mkutano huo na mwakilishi wake kwenye ubalozi wake jijini Abuja, Kanali Soumana Kalkoye.

Wakuu hao wa Majeshi kutoka nchi za Afrika, wanajadili namna ya kuja na mbinu kama waafrika kupambana na changamoto za kiusalama zinazoendelea kushuhudiwa.

Katika hotuba yake ya ufunguzi, mwenyeji wa mkutano huo, Mkuu wa Majeshi wa Nigeria, Jenerali Christopher Musa amesema mataifa ya Afrika yanapaswa kuja na mbinu mpya na ya pamoja, ili kupambana na changamoto za kiusalama.

Kanda zote za Afrika zinakabiliwa na utovu mkubwa wa usalama, baada ya kuibuka kwa makundi ya kijihadi na kigaidi, yanayopambana na serikali na kusababisha mauaji ya raia wa kawaida.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *