Aliongeza kuwa Wizara ya Fedha imeidhinisha bajeti ya dharura ya dola milioni 18.7 ili kuushughulikia mzozo huo. Rais Duma Boko alisema jeshi litasimamia usambazaji wa dawa za dharura, huku shehena za kwanza zikiondoka mara moja katika mji mkuu wa Gaborone na kuyapa kipaumbele maeneo ya vijijini ambayo hayajahudumiwa.

Tangu kuanza kwa mwezi huu, Wizara ya Afya ilikuwa imeziagiza hospitali kuahirisha shughuli zisizo za lazima kwa sababu ya uhaba wa dawa. Botswana ni miongoni mwa mataifa kadhaa ya Afrika yaliyoathiriwa na hatua ya hivi karibuni ya serikali ya Marekani kupunguza misaada ya maendeleo katika sekta ya afya. Mgogoro huo pia unahusishwa na kupungua kwa bajeti ya taifa kulikosababishwa na kudorora kwa soko la almasi duniani. Botswana, yenye wakazi milioni 2.5 kusini mwa Afrika, ni mojawapo ya wazalishaji wakubwa wa almasi duniani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *