Rais Masoud Pezeshkian wa Iran amesema kuwa mazungumzo ya kidiplomasia hayatakuwa na maana iwapo kundi la nchi tatu za Ulaya E3 linaloundwa na Uingereza, Ufaransa na Ujerumani zitarejesha tena vikwazo dhidi ya Tehran.

Rais Pezeshkian ameeleza haya katika kmkutano na Rais wa Uswisi Karin Keller- Sutter pambizoni mwa Mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York. 

“Tunakaribisha mazungumzo ya kidiplomasia ili kutatua kadhia ya (nyuklia) lakini iwapo utaratibu wa vikwazo kwa jina la Snapback  utahuishwa mazungumzo hayatakuwa na maana tena,”amesema Rais wa Iran. 

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameongeza kuwa hukmu ya kidini iliyotolewa na Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei inakataza uundaji wa silaha za nyuklia. Amesisitiza kuwaIran iko tayari kuthibitishwa suala hili katika fremu ya sheria za kimataifa na haki zake. 

Nchi tatu za Ulaya zilizotia saini makubaliano ya nyuklia mwaka 2015  kwa jina la Mpango Kamili wa Utekelezaji wa Pamoja (JCPOA) mwezi Agosti mwaka huu zilianzisha utaratibu wa papo kwa hapo au Snapback zikisema kuwa zinatiwa wasiwasi na madai yanayotolewa kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran.

Irankwa upande wake imepinga hatua hiyo iliyo kinyume cha sheria ya Troika ya Ulaya na kuzituhumu nchi hizo tatu kwa kuunga mkono vikwazo haramu badala ya kutekeleza ahadi zao kwa mujibu wa makubaliano ya JCPOA.  

Katika mazungumzo hayo huko New York, Rais wa Uswisi amesema kuwa nchi yake inakaribisha ushirikiano wowote wenye kujenga kati ya Iran na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA).

Rais Keller- Sutter ameongeza kuwa Bern inaamini pakubwa kwamba mazungumzo ya kidiplomasia ni njia bora ya kuzipatia ufumbuzi kadhia mbalimbali.  

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *