
Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia amesema kuwa nchi yake inaendelea kutiwa wasiwas sana na mateso na masaibu wanayopitia wananchi wa Palestina na kutaka kufikia mapatano ya kusimamisha vita haraka iwezekanavyo katika Ukanda wa Gaza.
Rais wa Somalia ametoa wito wa kufikiwa usitishaji vita wa haraka na wa kudumu, kuruhusiwa misaada ya kibinadamu kuingia Gaza na kuhuhuishwa juhudi za kutafuta suluhu ya nchi mbili kama njia pekee inayowezekana kwa ajili ya haki na amani ya kudumu katika eneo la Mashariki ya Kati hii leo.
Rais Hassan Sheikh Mohamud amesema kuwa Somalia ambaye si mwakilishi wa kudumu wa Baraza la Usalama imekuwa ikifanya kazi bla kuchoka ili kuhakikisha kuwa amani, utulivu na fursa za pamoja zinapatikana kote ulimwenguni.
Katika kukabiliana na makundi ya kigaidi, Rais wa Somalia amewasifu washirika wa kimataifa wa nchi hiyo ya Afrika Mashariki katika mapambano yake dhidi ya ugaidi na kuvipongeza vikosi vya usalama vya Somalia kwa “kujitolea na ujasiri usioyumba” dhidi kundi la kigaidi la al-Shabaab na ISIS (Daesh).
Rais wa Somalia ameyataja makundi hayo ya kigaidi kuwa taasisi hatari zaidi za kigaidi duniani.