
Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Msaada kwa Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA), Philippe Lazzarini, ametoa onyo kali kuhusu hali ya kibinadamu ya Gaza kiasi kwamba Wapalestina wanafadhilisha kufa kulika kuishi kwa mateso wakati huu utawala katili wa Israel unaendeleza vita vya maangamizi ya kimbari katika eneo hilo.
Siku ya Alhamisi, Lazzarini aliwaambia waandishi wa habari katika mkutano wa waandishi uliofanyika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York kwamba hali Gaza bado ni “haiwezi kuvumilika kabisa,” akieleza mazingira hayo kama “jahanamu kwa sura zake zote zinazowezekana.”
Lazzarini alisema: “Nadhani ni muhimu daima, siku baada ya siku, kujikumbusha kuhusu kinachoendelea kule, ili kuhakikisha hatuanzi kuhisi kama kimepitwa na wakati au kutokuwa na hisia”
Alisema hali ni mbaya kiasi kwamba “ni jambo la kawaida sasa Gaza kusikia watu wakisema ndoto yao ni kufa kwa heshima, badala ya kupitia mateso haya.”
“Nadhani ni muhimu sana kuendelea kuonyesha hasira kamili juu ya kinachoendelea, na bila shaka, sehemu ya kuchanganyikiwa kwetu ni kwamba hasira hii haijatafsiriwa bado kuwa hatua madhubuti ya kumaliza ukatili tunaorekodi kila siku.”
Lazzarini aliwataka viongozi wa dunia wachukue hatua. Alisema darasa zima la watoto hufa kila saa, huku kiasi kikubwa cha chakula kikiwa kimezuiliwa nje ya Gaza.
Alikosoa kile kinachoitwa Taasisi ya Misaada ya Kibinadamu inayofadhiliwa na Israel na Marekani, akiikitaja kama chombo cha malengo ya kisiasa na kijeshi.
Lazzarini alisema mfumo wa kibinadamu unaporomoka Gaza, huki akimtaka Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, kumaliza jahanamu hii.
Alisisitiza kuwa ni uamuzi wa kisiasa pekee unaoweza kusitisha mateso ya Wapalestina katika eneo hilo na kurejesha upatikanaji wa msaada wa maana.
Lazzarini alithibitisha dhamira ya UNRWA ya kuwatumikia Wapalestina. “Bado tunafanya kazi Gaza. Bado tunao wafanyakazi 12,000.”
Vita vya mauaji ya kimbari vya Israel dhidi ya Gaza vilianza tarehe 7 Oktoba 2023, baada ya wapigania ukombozi wa Palestina kutekeleza Operesheni Kimbunga cha Al-Aqsa dhidi ya utawala wa kikoloni wa Israel, kama majibu kwa kampeni yake ya miongo ya utawala huo ya ukatili na uharibifu dhidi ya Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi.
Mashambulizi ya umwagaji damu ya utawala wa Kizayuni katika ukanda uliozingirwa yameua zaidi ya Wapalestina 65,500, wengi wao wanawake na watoto, huku maelfu zaidi wakihofiwa kuzikwa chini ya majengo yaliyobomolewa.