Leo ni Jumamosi tarehe 4 Mfunguo Saba Rabiul-Thani 1447 Hijria Qamaria, sawa na tarehe 5 Mehr mwaka 1404 Hijria Shamsia, inayosadifiana na tarehe 27 Septemba 2025 Miladia.
Katika siku kama ya leo, miaka 173 iliyopita, tarehe 4 Rabiu-Thani 1274 Hijria Qamaria, alizaliwa katika mji wa Madina Mtukufu Abdul Adhim Hassani, anayetokana na kizazi cha Imam Hassan Mujtaba (AS). Alikuwa mtu mwanafikra na mchamungu. Abdul Adhim Hassani alikuwa mmoja wa wapokezi wa Hadithi aliyekuwa akiaminiwa na Imam Hadi (AS). Mtukufu Abdul Adhim amesimulia Hadithi zinazotoka moja kwa moja kwa Maimamu watukufu kama vile Imamu Reza (AS), Imamu Jawad (AS), na Imamu Hadi (AS). Wakati wa Uimamu wa Imam Hadi (AS), Abdul Adhim Hassani alihajiri kuelekea Iran kwa ushauri wa Imam huyo mtukufu ili kuwaelekeza watu kwenye uongofu na akaweka maskani yake katika mji wa Rey, karibu na Tehran ya sasa. Haram toharifu ya mtukufu Abdul Adhim Hassani iko pia katika mji huo wa Rey na ni moja maeneo yanayopokea wafanya ziara wengi.

Siku kama ya leo miaka 40 iliyopita wapiganaji shujaa wa Iran walifanikiwa kuvunja mzingiro wa mji wa Abadan katika operesheni ya haraka na iliyokuwa imeratibiwa vyema dhidi ya ngome za jeshi la Saddam Hussein wa Iraq. Operesheni hiyo ilitekelezwa na wapiganaji wa Iran kufuatia agizo la Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu Imam Khomeini, Mwenyezi Mungu Amrehemu. Mji wa Abadan ulikuwa umezingirwa na wanajeshi wa Iraq kwa karibu mwaka mmoja tangu kuanza vita vya kulazimishwa vya utawala wa dikteta Saddam dhidi ya Iran.

Tarehe 27 Septemba inasadifiana na Siku ya Kimataifa ya ‘Utalii. Utalii ni moja ya sekta muhimu za mabadilishano ya kiutamaduni baina ya watu wa mataifa mbalimbali. Aidha utalii unaweza kutimia kupitia safari na utalii wa ndani na nje ya nchi kwa madhumuni tofauti. Licha ya kwamba utalii umekuwa na historia ya muda mrefu katika maisha ya mwanadamu, lakini utalii wa mfumo wa kisasa ulianza mwanzoni mwa karne ya 16, wakati yaliposhika kasi mapinduzi ya kiviwanda barani Ulaya na kuvumbuliwa aina mpya ya maisha barani humo.

Na siku kama ya leo miaka 72 iliyopita, mji wenye jamii kubwa ya watu wa Beijing ulichaguliwa rasmi kuwa mji mkuu wa China. Mji wa kihistoria wa Beijing unapatikana mashariki mwa nchi hiyo na unahesabiwa kuwa moja ya vituo vikubwa vya kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni nchini China. Beijing ilichaguliwa kuwa mji mkuu wa China baada ya Mao Tse-tung kuchukua madaraka ya nchi na kiongozi wa wakati huo wa China Chiang Kai-shek kulazimika kukimbilia Taiwan.
