
Rais wa Marekani Donald Trump amesema siku ya Jumatatu, Agosti 25, kwamba Wamarekani wengi “wangependa kuwa na dikteta,” wakati wa mkutano wa ghafla na waandishi wa habari na ambao ulirefushwa katika Ofisi ya Oval, uliozingatia masuala ya usalama na lawama dhidi ya wapinzani wake.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
“Watu wengi wanasema, ‘Labda tungependa kuwa na dikteta.’ Sipendi madikteta. Mimi si dikteta. Mimi ni mtu mwenye busara na akili,” amesema rais huyo wa Marekani, ambaye amekuwa akishutumiwa na wapinzani wake kwa mienendo ya kimabavu juu ya sera zake za uhamiaji na usalama.
“Watu wengi husema, ‘labda tungependa kuwa na dikteta.’ Sipendi madikteta mimi si dikteta mimi ni mtu mwenye busara na akili,” amesema rais huyo wa Marekani, akishutumiwa na wapinzani wake kwa ubabe juu ya sera zake za uhamiaji na usalama.
“Unatuma jeshi, na badala ya kukupongeza, wanakushutumu kwa kuvamia jamhuri,” amesema, akimaanisha uamuzi wake wa kutuma kikodi cha Walinzi wa taifa katika mitaa ya Washington kwa operesheni za kurejesha usalama.
Donald Trump alitia saini agizo la kiutendaji mbele ya waandishi wa habari likimuadhibu mtu yeyote anayechoma bendera ya Marekani, licha ya Mahakama ya Juu kutoa uamuzi mwaka 1989 kwamba kitendo hicho kiko chini ya uhuru wa kujieleza, haki ya msingi inayolindwa na Katiba. “Ukichoma bendera, utapata kifungo cha mwaka mmoja, bila kuachiliwa mapema,” alisema.
“Idara ya vita” ya baadaye
Rais huyo kutoka chama cha Republican mwenye umri wa miaka 79, ambaye alizungumza kwa dakika 80 juu ya mada mbali mbali, na hitilafu nyingi, pia amebaiisha kwamba anakusudia kuipa Wizara ya Ulinzi jina la “Wizara ya Vita.”
Donald Trump pia amewashambulia wapinzani wake wa kisiasa, haswa wale ambao wakati mwingine walitajwa kuwa wagombea wa uteuzi wa urais wa chama cha Democratic mnamo mwaka 2028. Hasa, alimwita Gavana wa Illinois kutoka chama cha Democrativ, J.B. Pritzker, kuwa ni “mcheshi” na akasema anapaswa “kufanya bidii zaidi,” akirejelea safu yake.
Donald Trump pia amemkosoa Gavana wa California Gavin Newsom na Gavana wa Maryland Wes Moore, ambao wote walimshambulia hivi majuzi kwa dhihaka kwenye mitandao ya kijamii. Kuhusu Chama cha Democratic, amesema, “Wagombea wao wote wanafanya kazi mbaya.” Rais pia hakumwacha mtangulizi wake wa chama cha Democratic, Joe Biden, ambaye alimwita “mpuuzi.”
Rais wa Marekani amekariri kwamba Chicago, Illinois, inaweza kulerngwa katika siku za usoni na operesheni zake za usalama zinazohusisha jeshi, baada ya Washington, D.C.
“Wanajua jinsi ya kujifanya kuwa wazuri!”
Mji mkuu wa shirikisho utakuwa “mkamilifu” kuandaa Kombe la Dunia msimu ujao wa joto, ametangaza Donald Trump. Amechukua fursa hiyo kuonyesha kombe la shindano hilo, lililoletwa kwake na mkuu wa FIFA Gianni Infantino na sasa ametawazwa katika Ofisi ya Oval, kati ya mapambo mengine yaliyopambwa.