fg

Serena Williams, Elon Musk na Whoopi Goldberg wote wamezungumza kuhusu kutumia sindano za kupunguza uzito. Baadhi ya sindano hizo zinakubaliwa na Taasisi ya Kitaifa ya Afya ya Uingereza (NHS), ikiwa ni pamoja na sindano ya Wegovy na Mounjaro, ambazo ni maarufu zaidi.

Takriban watu milioni 1.5 nchini Uingereza hutumia sindano hizi – lakini zaidi ya tisa kati ya 10 wanaaminika kufanya malipo katika hospitali binafsi. Bei hutofautiana lakini kwa ujumla hugharimu kati ya pauni 100 na 350 kwa mwezi, kulingana na kipimo na usaidizi unaouhitaji.

“Hatuwezi kuruhusu afya kuwa anasa kwa matajiri,” anasema Katharine Jenner, mkurugenzi mtendaji wa Obesity Health Alliance.

Je, ni kweli kwamba sindano za kupunguza uzito – zinageuza suala la kupunguza unene kuwa suala la matajiri pekee?

Pia unaweza kusoma

Zinafanyaje kazi?

CV

Chanzo cha picha, Getty Images

Dawa za kupunguza uzito zimekuwa zikipatikana kwenye hospitali za NHS kwa muda mrefu, lakini mazingira yalibadilika baada ya kuanzishwa kwa baadhi ya dawa mpya – miongoni mwazo, semaglutide, chini ya jina Wegovy, na tirzepatide, zinazouzwa kama Mounjaro.

Wegovy ilitolewa na NHS kwa mara ya kwanza kwa watu wanene mwaka 2023, huku Mounjaro ikitolewa mapema mwaka huu. Hufanya kazi ya kizuia hamu ya kula, na kumfanya mtu kujisikia ameshiba.

Uchunguzi umeonyesha watu wanene wanaweza kupoteza hadi asilimia 20 ya uzito wa mwili.

“Tumepata janga la unene wa kupindukia na dawa hizi hutupatia fursa ya kukabiliana nalo kwa njia ambayo hatujawahi kufanya hapo awali. Lakini uwezo wako wa kufaidika unategemea zaidi kama una uwezo wa kulipa,” anasema Martin Fidock, mkurugenzi wa Ovivia, kampuni inayotoa sindano ya Wegovy na ushauri kuhusu mtindo wa maisha kwa wagonjwa wa NHS.

Kinachoongeza changamoto ni ukweli kwamba watu wengi kutoka katika maeneo masikini wanakabiliwa na unene wa kupindukia: zaidi ya theluthi moja ya watu katika maeneo masikini ni wanene kupita kiasi – mara mbili ya vitongoji tajiri.

Kuna hatari nyingi za kiafya kwa watu wanene, ikiwa ni pamoja na hatari ya kupata saratani na ugonjwa wa moyo, pamoja na matatizo ya afya ya akili. Pia zipo athari za kijamii.

Utafiti mmoja nchini Marekani uligundua kuwa wanaume wanene walio na shahada ya kwanza hupata 5% ya mshahara chini ya wenzao wembamba wenye elimu sawa na wao.

Kwa wanawake wanene, hali ni mbaya zaidi, hupata chini ya 12%, kulingana na data kuhusu wafanyakazi 23,000 wa Marekani, iliyochapishwa katika The Economist mwaka 2023.

Tatizo la gharama

FGV

Chanzo cha picha, Getty Images

18% ya Waingereza wenye uzito uliopitiliza wako tayari kulipia dawa za kupunguza uzito – lakini kama dawa hizo zinapatikana kwenye hospitali za NHS, kulingana na utafiti wa wakala wa mawasiliano wa Strand Partners.

Na baadhi ya wale walio tayari kulipa wanahofia kulipa gharama kubwa.

“Kama nitalazimika kulipa pauni 300 au zaidi, nitangaika sana kumudu,” anasema Pete Beech, 57, kutoka Southampton.

James O’Loan, mkuu wa duka la dawa la mtandaoni 4 U, anasema, “watu wengi hawawezi kuendelea na dozi kwa sababu ya gharama.”

Lakini haya yote yanaleta swali pana zaidi – katika mijadala ya kimatibabu kuhusu kukabiliana na unene wa kupindukia.

“Kwa uwepo wa matibabu ya unene: Je, watu wataacha kufikiria kuhusu suala gumu zaidi ambalo ni udhibiti wa chakula, ambalo ndiyo sababu kuu ya unene,” anauliza Greg Fell, rais wa Chama cha Wakurugenzi wa Afya ya Umma.

Nchini Uingereza baada ya vita, unene uliokithiri ulikuwa nadra kutokana na uhaba wa chakula – makundi ya watu wenye kipato cha chini yalikuwa na uwezekano mkubwa wa kukumbwa na utapiamlo.

Lakini tangu miaka ya 1980 viwango vya unene wa kupindukia vimeongezeka katika tabaka zote za kijamii, matajiri na maskini.

Watu katika maeneo maskini wamezingirwa na vyakula ovyo ovyo, vyakula visivyofaa, na wanakabiliwa na shida kubwa ya kutoweza kununua chakula chenye afya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *