Abbas Araqchi Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa makubaliano kuhusu utaratibu kwa jina la “Snapback” hayakufikiwa mjini New York kutokana na matakwa ya kupindukia ya Marekani, ikiungwa mkono na nchi za Ulaya.

Akizungumza na waandishi wa ihabari kabla ya kuondoka New York jana Jumatatu, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran alieleza kuhusu safari yake ya kidiplomasia iliyojumuisha majadiliano kwa ajili ya kuzuia kurejeshwa vikwazo vya Umoja wa Mataifa, kushiriki kwake katika Mkutano wa Baraza Kuu la UN na vikao vingine vya kimataifa na mikutano mbalimbali ndani na nje ya Umoja wa Maaifa. 

Sayyid Abbas Araqchi ameitaja hatua ya pande za Ulaya kuwa ni jaribio lililotekelezwa ili Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ifikie makubaliano yasiyo na maana.

Amesema kuwa, Iran iliwasilisha mapendekezo yake ya kimantiki kikamilifu ambayo pande za Ulaya pia zilikiri kuwa ni ya yanayostahiki.

Tarehe 19 mwezi huu wa Septemba nchi 15 wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa zilishindwa kuidhinisha azimio ambalo lingezuia kurejeshewa vikwazo Iran baada ya nchi tatu za Ulaya kuchochea utaratibu wa Snapback na kuituhumu Tehran kuwa imeshindwa kufungamana na makubaliano ya JCPOA. 

Ijumaa iliyopita pia Baraza la Usalama lilishindwa kupasishwa azimio ambalo lingepelekea kurefushwa kwa muda wa miezi sita makubaliano ya JCPOA na kwa azimio nambari 2231 la baraza hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *