.

Chanzo cha picha, Getty Images

Manchester City na Real Madrid wanamfuatilia winga wa Ufaransa Michael Olise huku Bayern Munich wakifikiria kumpa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 mkataba ulioboreshwa. (Team Talks)

Tottenham wanatazamiwa kukubaliana kandarasi mpya na kiungo wa kati wa Uruguay Rodrigo Bentancur, 28, ambaye mkataba wake wa sasa unakamilika msimu wa joto wa 2026. (Athletic – Subscription Required)

Arsenal wako tayari kumlipa mshambuliaji wa Uingereza Bukayo Saka, 24, ambaye kandarasi yake inakamilika msimu wa joto wa 2027, zaidi ya pauni 250,000 kwa wiki. (Sportsport)

Southampton wanapanga kumpa kiungo wa kati wa West Ham Muingereza James Ward-Prowse, 30, nafasi ya kurejea St Mary’s mwezi Januari. (GiveMesport)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Bayern Munich inanuia kumbakisha kwa mkopo mshambuliaji wa Chelsea na Senegal Nicolas Jackson, 24, kwa msingi wa kudumu hata kama masharti ya wajibu wa kumnunua kwenye mkataba wake hayatatimizwa. (TBR Football)

Chelsea wana imani kuwa wataweza kumsajili mlinda lango wa AC Milan na Ufaransa Mike Maignan mwenye umri wa miaka 30. (ASRomalive – In Itali)

Tottenham, West Ham na Nottingham Forest wanavutiwa na mshambuliaji wa Parma raia wa Argentina Mateo Pellegrino, 23, lakini klabu hiyo ya Italia haitaki kumuuza kabla ya msimu ujao wa joto. (TuttoSport via Parma Live – Italy)

Liverpool wanaweza kuwa tayari kumruhusu mlinzi wa England Joe Gomez kuondoka mwezi Januari – mradi tu wanaweza kupata mbadala wake – huku AC Milan ikimtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28. (Caughtoffside)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Wakiwa wamekataliwa uchunguzi wa mkopo katika siku ya mwisho ya kuhama, Porto wanamfuatilia kwa karibu winga wa umri wa miaka 19 wa Brighton na England Chini ya 21 Tommy Watson. (Football Insider)

AC Milan wanavutiwa na mshambuliaji wa Barcelona na Poland Robert Lewandowski, 37. (Sport kupitia Tuttomercatoweb – In Italy)

Mshambulizi wa Argentina Julian Alvarez, 25, anasema haruhusu uvumi na Barcelona kumuathiri na analenga “kushinda” Atletico Madrid. (ESPN)

Imetafsiriwa na Seif Abdalla

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *