“FU-AES” inawakilisha kikosi kilichounganishwa cha Muungano wa Nchi za Sahel. Hili ndilo lilikuwa lengo la ziara ya Jenerali Abdourahamane Tiani mjini Bamako siku ya Jumanne, Septemba 30. Mkuu wa nchi wa Niger alipokelewa na mwenzake wa Mali, Jenerali Assimi Goïta. Kufuatia mkutano wao, Abdourahamane Tiani alibainisha kwamba makao makuu ya pamoja ya jeshi sasa yanafanya kazi na kwamba bataliano za kwanza zimeundwa.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Makao makuu  ya FU-AES yako Niamey, Niger, ndani ya kambi ya wanahewa ya 101—ambayo awali ilitumiwa na kikosi cha Operesheni Barkhane.

Kikosi hiki kinaongozwa na afisa wa Burkina Faso: Kanali Éric Dabiré, kamanda wa zamani wa kanda ya 6 ya kijeshi mashariki mwa Burkina Faso, mojawapo ya maeneo yaliyoathiriwa zaidi na mashambulizi ya kigaidi.

Vifaa na maandalizi ya vikosi

Kama makao makuu inafanya kazi, “wakati umefika wa kuandaa vitengo.” Siku ya Jumapili, Septemba 28, Rais wa Burkina Faso Ibrahim Traoré alisema kwamba “kila nchi ya AES inaagiza vifaa,” ambavyo vinashirikiwa.

Kulingana na Rais Ibrahim Traoré, “kikosi cha kwanza cha Burkina Faso kiko tayari,” wakati ” cha pili  kinapewa mafunzo na kinapaswa kufanya kazi ndani ya miezi miwili.”

Operesheni za pamoja tayari zinaendelea

Tangu mwezi Januari 2025, wakati uundaji wa FU-AES ulipotangazwa, shughuli za pamoja zilifanyika. Hatimaye, kikosi hicho kinatarajiwa kujumuisha takriban wanajeshi 5,000 kutoka majeshi ya Mali, Niger, na Burkina Faso.

Kabla ya kurejea Niamey, Abdourahamane Tiani alisimama kwa muda huko Ouagadougou, Burkina Faso, ambako alikutana na Rais Ibrahim Traore.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *