.

Chanzo cha picha, Reuters

Uwanja wa
ndege wa Munich nchini Ujerumani umefuta safari zaidi ya kumi na mbili baada ya
ndege zisizo na rubani kuonekana karibu na anga yake.

Takriban
safari 17 za ndege zilisitishwa mjini Munich, na kuathiri takriban abiria
3,000.

Uwanja wa
ndege wa Munich ulisema ulielekeza safari 15 za ndege kwenda miji ya karibu.

Hakukuwa na
uthibitisho wa haraka wa wapi ndege hizo zisizo na rubani zilitoka. Viwanja vya
ndege kadhaa kote barani Ulaya vimefungwa katika wiki za hivi karibuni kwa
sababu ya ndege zisizo na rubani ambazo hazijatambuliwa.

Uwanja wa
ndege wa Munich ulitoa taarifa kwa mamlaka baada ya ndege hizo kugunduliwa.

Safari za
ndege kutoka uwanja wa ndege wa Munich “zimesimamishwa”, uwanja
wa ndege ulisema.

Udhibiti wa
trafiki ya anga ulielekeza upya safari za ndege ambazo zilipaswa kutua Munich
hadi Stuttgart, Nuremberg, Vienna na Frankfurt.

Kwa sababu
kulikuwa na giza, hakuna habari kuhusu aina, ukubwa au asili ya ndege hizo
zisizo na rubani zilizothibitishwa, msemaji wa Polisi wa Shirikisho Stefan
Bayer aliliambia Gazeti la Bild. Ndege zisizo na rubani zilionekana kwa mara ya
kwanza saa 21:30 kwa saa za eneo (19:30 GMT), na kisha tena saa moja baadaye,
polisi walisema.

BBC
imewasiliana na polisi wa jimbo la Bavaria na polisi wa shirikisho la
Ujerumani.

Pia unaweza kusoma:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *