.

Chanzo cha picha, Getty Images

    • Author, Angus Crawford
    • Nafasi, BBC

Kanuni za TikTok zinapendekeza ponografia na maudhui yenye ngono kwa akaunti za watoto, kulingana na ripoti mpya ya kikundi cha kampeni ya haki za binadamu.

Watafiti waliunda akaunti ghushi za watoto na kufungua mipangilio ya usalama lakini bado walipokea mapendekezo ya utafutaji wa video za ngono.

Hoja za utafutaji zilizopendekezwa zilisababisha nyenzo za ngono zikiwemo video chafu .

Jukwaa hilo hatahivyo linasema limejitolea kuweka usalama unaolingana na umri na lilichukua hatua mara moja lilipogundua tatizo.

Mwishoni mwa mwezi Julai na mapema Agosti mwaka huu, watafiti kutoka kikundi cha kampeni cha Global Witness walianzisha akaunti nne kwenye TikTok wakijifanya kuwa na umri wa miaka 13.

Walitumia tarehe za uwongo za kuzaliwa na hawakuulizwa kutoa taarifa nyingine yoyote ili kuthibitisha utambulisho wao.

Picha za ngono

Pia walifungua “hali yenye vikwazo” au restricted mode ya jukwaa hilo, ambayo TikTok inasema inazuia watumiaji kuona “mandhari ya watu wazima au maudhui mazito, kama vile… yale yanayochochea ngono”.

Bila kufanya utafutaji wowote, wachunguzi walibaini hoja za utafutaji zenye kujamiiana kupita kiasi zikipendekezwa katika sehemu ya “unaweza kupenda” ay {You may like} ya programu.

Maneno hayo ya utafutaji yalionesha maudhui ya wanawake wanaoiga punyeto.

Video nyingine zilionyesha wanawake wakiangaza chupi zao katika maeneo ya umma au kuonesha maziwa yao.

Katika hali yake ya kupita kiasi, maudhui yalijumuisha filamu chafu za ponografia za ngono.

Video hizi zilipachikwa katika maudhui mengine yasiyo na hatia katika jaribio la kuzuia udhibiti wa maudhui.

Ava Lee kutoka Global Witness anasema matokeo hayo yalikuja kama “mshtuko mkubwa” kwa watafiti.

“TikTok sio tu inashindwa kuzuia watoto kufikia maudhui yasiyofaa – inawapendekezea mara tu wanapofungua akaunti”.

Global Witness ni kikundi cha kampeni ambacho kwa kawaida huchunguza jinsi teknolojia kubwa inavyoathiri mijadala kuhusu haki za binadamu, demokrasia na mabadiliko ya hali ya hewa.

Watafiti waligundua tatizo hili wakati wakifanya utafiti mwingine mwezi Aprili mwaka huu.

Video zaondolewa

Waliarifu TikTok, ambayo ilisema ilikuwa imechukua hatua za haraka kutatua tatizo hilo.

Lakini mwishoni mwa Julai na Agosti mwaka huu, kikundi cha kampeni kilirudia zoezi hilo na kugundua kwa mara nyingine kuwa programu hiyo ilikuwa inapendekeza maudhui ya ngono.

TikTok inasema kuwa ina zaidi ya vipengele 50 vilivyoundwa ili kuwaweka vijana salama: “Tumejitolea kikamilifu kutoa matumizi salama na yanayolingana na umri”.

Programu hiyo inasema inaondoa video tisa kati ya 10 zinazokiuka mwongozo wake kabla hazijatazamwa.

Ilipofahamishwa na Global Witness kuhusu matokeo yake, TikTok inasema ilichukua hatua “kuondoa maudhui ambayo yalikiuka sera zetu na kuzindua uboreshaji wa kipengele chetu cha mapendekezo ya utafutaji”.

Kanuni za Watoto

Mnamo tarehe 25 Julai mwaka huu, Kanuni za Watoto za Sheria ya Usalama Mtandaoni zilianza kutumika, na kuweka wajibu wa kisheria wa kuwalinda watoto mtandaoni.

Majukwaa sasa yanapaswa kutumia “uhakikisho bora wa umri” ili kuzuia watoto kuona ponografia. Ni lazima pia warekebishe kanuni zao ili kuzuia maudhui ambayo yanahimiza kujidhuru, kujiua au matatizo ya kula.

Global Witness ilifanya mradi wake wa pili wa utafiti baada ya Kanuni za Watoto kuanza kutumika.

Ava Lee kutoka Global Witness alisema: “Kila mtu anakubali kwamba tunapaswa kuwaweka watoto salama mtandaoni… Sasa ni wakati wa wadhibiti kuingilia kati.”

Wakati wa uchunguzi wao, watafiti pia waliona mwitikio wa watumiaji wengine kwa maneno ya utafutaji ya ngono waliyokuwa wakipendekezewa.

Mtoa maoni mmoja aliandika: “Je! kuna mtu anaweza kunielezea ni nini kinachoendelea katika utaftaji wangu pls?”

Mwingine aliuliza: “ni nini kibaya na programu hii?”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *