Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) imeongeza muda wa udahili wa shahada ya kwanza katika programu ambazo bado zina nafasi kwa mwaka wa masomo 2025/2026. Hatua hiyo inalenga kutoa nafasi kwa wanafunzi ambao hawakufanikisha kutuma maombi kwenye dirisha la kwanza na la pili.
Kwa mujibu wa TCU, dirisha la udahili la awamu ya tatu litafunguliwa kuanzia Oktoba 6 -10 mwaka huu.
#AzamTVUpdates
Mhariri |John Mbalamwezi