Mgombea wa ubunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel Nuwas, amemuomba mgombea urais wa Tanzania kw atiketi ya CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan endapo atachaguliwa, kusaidia wakulima na wafugaji wa jimbo hilo.
Amesema jimbo lake lina mabwawa yanayohitaji kusafishwa ili kunyweshea mifugo na kufanya umwagiliaji uwe na tija.
Aidha, amesisitiza tatizo la majosho na masoko katika miji ya Haydom na Dongobesh, ili wakinamama wapate fursa ya kuuza bidhaa zao.
✍ Hellen Kawiche
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates