Mgombea ubunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Mkinga, Twaha Mwakioja, ameahidi kushughulikia changamoto za msingi zinazowakabili wananchi wa jimbo hilo, zikiwemo huduma za afya, elimu na miundombinu ya barabara, endapo atapata ridhaa ya kuongoza.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Mayomboni, Mwakioja amesema dhamira yake ni kuendeleza mafanikio yaliyokwisha kuanzishwa na serikali ya CCM, huku akiwataka wananchi kukichagua chama hicho ili kuhakikisha maendeleo hayo yanaimarishwa na kufika kwa wananchi wengi zaidi.
✍ Mariam Shedafa
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates