
Akizungumza wakati wa sala ya kila wiki, Papa amezitaka pande zote kushiriki kikamilifu katika mchakato wa amani, akisisitiza hitaji la haraka la kuumaliza mzozo huo na kuanzisha “amani ya haki na ya kudumu”.
Wapatanishi wa Israel na Hamas wamekutana Jumapili mjini Cairo katika mazungumzo ya kujaribu kumaliza mzozo huo wa Mashariki ya Kati.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio amesema Israel na Hamas zimekubaliana kuhusu sehemu kubwa ya mpango huo wa amani uliopendekezwa na rais Donald Trump lakini akasisitiza kuwa suala la kundi hilo kupokonywa silaha ndio linalojadiliwa kwa sasa na linatarajiwa kuleta utata.