Mgombea Ubunge wa jimbo la Kibamba Angellah Kairuki ameiomba jamii ya Waislamu na wasio Waislam kuungana kwa pamoja kujenga jamii bora hususani kwenye misingi ya malezi ya watoto huku akiahidi kuhakikisha jimbo hilo linapata shule ya kuhudumia watoot wenye mahitaji maalum.
Kairuki akizungumza katika Kongamano la Waumini Wa Kiislam lililofanyika Dar e Salaam na kuongozwa na kauli mbiu ya ‘Jitambue, Badilika, Acha Mazoea’ ameongeza kuwa ni vyema wananchi wakashukuru kwa kuwa na Rais Samia Suluhu Hassan ambaye alikabidhiwa nchi katika wakati mgumu lakini majukumu ya kila nana aliyabeba na kuhakikisha mafanikio ya nchi yanaendelea kusonga mbele.
Mhariri @moseskwindi