
Katika taarifa yake ya jana Jumapili, serikali ilisema hakuna raia wala maafisa wa usalama waliouawa katika makabiliano hayo ya Jumamosi, ambayo kundi la wapiganaji wa al-Shabaab lenye mahusiano na al-Qaeda lilihusika.Serikali ilisema hakuna mfungwa yeyote aliyeweza kutoroka kutoka gereza la Godka Jilacow wakati wa shambulio hilo.Somalia imekuwa na utulivu kwa kiasi fulani katika miezi ya hivi karibuni, ambapo vikosi vya serikali vikisaidiwa na wanamgambo wa ndani na wanajeshi wa Umoja wa Afrika, wakiwasogeza wapiganaji wa al-Shabaab kutoka maeneo kadhaa ya kati na kusini mwa Somalia.