
Kesho Jumanne itakuwa inatimia miaka miwili tangu shambulio la Hamas lililoanzisha vita. Rais wa Marekani Donald Trump amepongeza tamko la Hamas linalokubali baadhi ya vipengele vya mpango wa amani wa Marekani. Israel imesema inaunga mkono juhudi mpya za Marekani. Kwa mujibu wa mpango huo, Hamas itawaachilia mateka 48 waliobaki, ikiwa takriban 20 wanaaminika kuwa hai ndani ya siku tatu. Pia itakubali kuachia madaraka na kusalimisha silaha. Kwa mujibu wa ofisi ya Netanyahu, ujumbe wa Israel unaoongozwa na mpatanishi mkuu Ron Dermer leo hii unatarajiwa kuwasili Sharm el-Sheikh kwa mazungumzo hayo. Na duru kutoka Misri zinasema ujumbe wa Hamas tayari umefika.