Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC, Jumatatu hii inatazamiwa kutoa uamuzi wake dhidi ya kiongozi wa wanamgambo nchini Sudan anayetuhumiwa kwa makosa ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu wakati wa mshambulio mabaya jmboni Darfur.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Ali Muhammad Ali Abd-Al-Rahman maarufu kama nom de guerre Ali Kushayb, anakabiliwa na makosa 31ya uhalifu ikiwemo ubakaji, mauaji na mateso yaliotekelezwa jimboni Darfur kati ya 2003 hadi Aprili 2004.

Waendesha mashtaka wanasema alikuwa kiongozi wa kundi la wanamgambo wa Janjaweed, ambao walishiriki katika vitendo kadhaa vya uhalifu wa kivita.

Mnamo Disemba 2024, Abd-Al-Rahman alikana mashataka yote dhidi yake huku pia akikana kuwa Ali Kushayb.

Ali Muhammad Ali Abd-Al-Rahman anadaiwa kuwa alitorokea nchini Jamhuri ya Afrika ya kati mnamo Februari 2020 baada ya serikali mpya ya Sudan kutangaza nia ya ya kushirikiana na mahakama ya ICC katika uchunguzi.

Aidha alisema uamuzi wake wa kujisalimisha ulitokana na hofu ya kukamatwa na kuuawa na serikali ambayo ilikuwa inamtafuta.

Vilevile, Abd-Al-Rahman anadaiwa kuwa mshirika wa karibu wa kiongozi aliyeondolewa madarakani dikteta Omar al-Bashir ambaye anatafutwa na ICC kwa makosa ya mauaji ya kimbari.

Umoja wa mataifa unasema takriban watu 300,000 waliuawa na wengine milioni 2.5 waliyahama makazi yao wakati wa vita vya Darfur miaka ya Elfu mbili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *