Nchini Madagascar, maafisa wa usalama, wanatetea uamuzi wao wa kutumia nguvu dhidi ya waandamanaji vijana maarufu kama Gen Z kwa madai kuwa, wanazua vurugu, badala ya kuandamana kwa amani.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kwa wiki ya pili sasa, waandamanaji wamekuwa wajitokeza kwenye miji mbalimbali, likiwemo jiji kuu Antananarivo, kulalamikia uhaba wa maji na kukatika kwa umeme mara kwa mara.

Polisi na maafisa wa jeshi ambao kwa pamoja, wamekuwa wakishirikiana kupambana na waandamanaji hao, katika ripoti ya pamoja, wanadai, waandamanaji hao wamekataa kufuata utaratibu wa kuandamana, hali ambayo imesababisha makabiliano makali.

Mmoja wa waandamanaji akiwa amekamatwa na maofisa wa usalama nchini Madagascar.
Mmoja wa waandamanaji akiwa amekamatwa na maofisa wa usalama nchini Madagascar. REUTERS – Zo Andrianjafy

Kufikia mwishoni mwa wiki iliyopita, watu 22 wameuawa na mamia kujeruhiwa, baada ya kuanza kwa maandamano hayo Septemba tarehe 25. Hata hivyo, serikali imekanusha kuhusu idadi hiyo ya watu waliopoteza maisha kwa kupigwa risasi na maafisa wa usalama.

Umoja wa Mataifa na watetezi wa haki za binadamu, wamelaani hatua ya maafisa wa usalama kutulia nguvu kupita kiasi na badala yake kutoa ulinzi kwa waandamanaji ili kupaza sauti zao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *