Mwishoni mwa hadhira kuu ya kila wiki siku ya Jumatano, Agosti 27, Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Leo XIV ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa na hasa ameiomba Israel kuheshimu sheria za kimataifa za kibinadamu.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mbele ya waumini 15,000, Papa ameomba kurejea kwa amani katika Ardhi Takatifu, na kutaka pande hasimu kuweka chini silaha zao, na kwamba jumuiya ya kimataifa iendelee kutoa shinikizo kukomesha mzozo wa Gaza. Amesikitishwa na vita ambavyo vimesababisha “ugaidi, uharibifu, na vifo vingi sana,” anaeleza mwandishi wetu wa Vatikani, Éric Sénanque.

Ingawa maneno yake yamekuwa ya tahadhari zaidi kuliko yale ya mtangulizi wake, Papa Francis, ambaye alitumia neno “mauaji ya halaiki” mwaka jana, Leo XIV hata hivyo ameizungumzia Israel waziwazi, bila kuitaja jina.

“Ninaomba kwamba mateka wote waachiliwe, usitishaji wa kudumu wa mapigano ukamilike, misaada ya kibinadamu iwezeshwe kuingia kwa usalama katika Ukanda wa Gaza, na sheria ya kibinadamu iheshimiwe kikamilifu, hasa wajibu wa kuwalinda raia na kujitenga na kuadhibu raia kwa pamoja, matumizi ya nguvu kiholela, na watu kulazimishwa kuhama,” Papa ameomba.

Leo XIV pia amerejelea maneno ya viongozi wa Kikristo wa Jerusalem, ambao, katika taarifa ya pamoja ya siku ya Jumanne, Agosti 26, walipinga vikali watu kuhamishwa kwa makusudi na kulazimishwa na kusisitiza haki ya Wapalestina kuishi katika ardhi yao wenyewe. “Hakuna kinachohalalisha kuwaweka raia kizuizini cha muda mrefu au kuwashikilia mateka katika mazingira mabaya,” walitangaza. “Sasa ni wakati wa kuponya familia ambazo zimeteseka kwa muda mrefu, kwa pande zote.” »

Tangu Oktoba 7, mashambulizi ya Israel yameua watu wasiopungua 62,895 huko Gaza, wengi wao wakiwa raia, kulingana na takwimu za Wizara ya Afya ya serikali ya Hamas.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *