Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha UDP, Saumu Hussein Rashid, amesema chama chake kina dhamira njema ya kuwaendeleza wajasiriamali na wafanyabiashara wadogo kwa kuwawekea miundombinu rafiki pamoja na kuwapatia mitaji itakayowawezesha kukuza kipato chao, lengo likiwa ni kuwainua kiuchumi.
Ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na wafanyabiashara wa Soko la Tibirinzi, Chake Chake, Mkoa wa Kusini Pemba, alipotembelea soko hilo kwa ajili ya kujionea hali ya miundombinu na mazingira ya biashara.
Mhariri | @claud_jm
#AzamTVUpdates