#HABARI: Mahakama Kuu ya Tanzania leo inatarajiwa kuanza kusikiliza kesi ya kupinga kuenguliwa kwa mgombea urais wa ACT-Wazalendo, Luhaga Mpina, hatua ambayo inaweza kubadili mwelekeo wa uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Kesi hiyo imepewa kipaumbele kwa maombi ya dharura yaliyowasilishwa na ACT-Wazalendo, ikidai uamuzi wa Msajili wa Vyama vya Siasa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) uliomnyima nafasi ya kugombea, ni kinyume cha sheria na haki za kidemokrasia.
Kwa mujibu wa mawakili wa chama hicho, mahakama leo itasikiliza hoja za awali zenye lengo la kuamua kama zuio hilo lilikuwa la kisheria, ama ni uamuzi wa kiutendaji uliopita mipaka ya kikatiba.
Iwapo Mpina atashinda shauri hili, anaweza kurejeshwa rasmi kwenye kinyang’anyiro cha urais na hivyo kuongeza ushindani katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025.
Lakini iwapo kesi hiyo itatupiliwa mbali, itathibitisha uchaguzi kufanyika bila ACT-Wazalendo kuwa na mgombea wa urais.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania