Kumezuka taharuki katika Mtaa wa Nzuguni B, jijini Dodoma kufuatia matukio ya ubakaji yanayodaiwa kufanywa na watu wanaovamia nyumba za wanawake usiku wakiwa na silaha za jadi.
Wananchi, hususan wanawake, wamelalamikia kuongezeka kwa matukio hayo, hali iliyolazimu serikali ya mtaa kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kuanzisha msako maalum. Hadi sasa, vijana 15 wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuhusika na matukio hayo huku uchunguzi ukiendelea.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi