Mgombea Urais kupitia Chama cha National League for Democracy (NLD), Doyo Hassan Doyo, ameahidi kujenga barabara 54 za juu jijini Dar es Salaam endapo atachaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Doyo amesema hatua hiyo inalenga kutatua changamoto sugu ya foleni za magari zinazolikabili jiji hilo, hususan katika maeneo yenye msongamano mkubwa wa magari.
Alitoa ahadi hiyo wakati wa mikutano yake ya kampeni katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Temeke.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi