Mke wa Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mariam Mwinyi, amewataka wanawake wa Kisiwa cha Pemba kuhakikisha wanatoa ushirikiano wa dhati kwa kumpa Dkt. Hussein Ali Mwinyi kura za kutosha katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Akizungumza kwenye mkutano wa wanawake ulioandaliwa na Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) katika uwanja wa Tibirizi, Wilaya ya Chake Chake, Mariam amesema kura hizo zitamwezesha Dkt. Mwinyi kuendeleza ajenda ya maendeleo kwa kipindi kingine cha miaka mitano.

Mariam amebainisha kuwa Serikali ya Dkt. Mwinyi imefanikiwa kutekeleza kwa mafanikio makubwa ilani ya CCM ya mwaka 2020 – 2025, hususan katika sekta za elimu, afya, uwezeshaji wanawake, na miundombinu.

Amesisitiza kuwa wanawake wamekuwa mashahidi wa huduma bora zinazotolewa na serikali ya CCM, hivyo ni jukumu lao kuhakikisha Dkt. Mwinyi anaendelea kuiongoza Zanzibar ili kuleta maendeleo zaidi.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *