Benki ya TCB imesema imekuja na mkakati wa kukuza uchumi na kuimarisha biashara ndogondogo na za kati kupitia huduma bunifu zinazolenga wajasiriamali na Watanzania wanaoishi nje ya nchi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam katika kikao na wateja, Mkurugenzi Mtendaji wa TCB, Jema Msuya amesema benki hiyo imezindua Stawi Bond, bidhaa mpya inayotoa riba ya hadi asilimia 13.5, ikilenga kuwapa wajasiriamali njia salama na yenye tija ya kuwekeza mitaji yao.

Ameongeza kuwa benki hiyo pia imeboresha huduma za diaspora, ikiwapa Watanzania wanaoishi nje urahisi wa kutuma, kuwekeza na kufuatilia fedha zao kwa njia za kidigitali, hatua itakayoongeza mzunguko wa fedha na uwekezaji wa ndani.

Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *