Watu wawili wanahofiwa kufariki dunia katika ajali iliyohusisha basi la kampuni ya Mallesa linalofanya safari kati ya Dar es Salaam na Geita, na lori lililokuwa limebeba vifaa mbalimbali vya ujenzi.

Ajali hiyo imetokea majira ya saa nane usiku wa kuamkia leo katika eneo la Kijiji cha Lumasa, Kata ya Butengolumasa, Wilaya ya Chato mkoani Geita.

Taarifa za awali kutoka kwa mashuhuda zinasema watu waliopoteza maisha wanadaiwa kuwa ni miongoni mwa waliokuwa ndani ya lori hilo, baada ya lori hilo kupasuka tairi ya mbele na kupoteza mwelekeo, kisha kugongana uso kwa uso na basi hilo lililokuwa likielekea Geita, zikiwa zimebaki kilomita chache kufika mjini Geita.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita alipoulizwa kwa njia ya simu amesema kwa sasa yupo safarini, na kwamba Kaimu RPC atatoa taarifa kamili.

✍ Ester Sumira
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *