Dunia inaungana Agosti 30 kuadhimisha siku ya watu waliopotea,takwimu zikisema kuna watu karibu laki tatu ambao hawajulikani waliko, kote ulimwenguni. Baadhi ya watu waliotenganishwa na wapendwa wao ni wakimbizi waliofurushwa makwao kutokana na vita au mizozo tofauti.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Katika kambi ya Kakuma 3 tulikutana na Amar Adam mkimbizi kutoka eneo la Darfur nchini Sudan ambaye alitenganishwa na ndugu zake tangu alipokimbia vita mwaka 2004.

Kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu ikishirikiana na Shirika la msalaba mwekundu nchini ,katika mpango maalum wa kurejesha na kudumisha uhusiano wa kifamilia ,zimekuwa kwenye mradi wa miaka kujaribu kuwaunganisha wakimbizi hao na wapendwa hao ili kuwapa hao ahueni.

Kwenye mpango huo,mkimbizi anaweza kuchagua kuandika ujumbe maalum kwa wapendwa wake ambao unatumwa kwa kwa ushirikiano wa ICRC na mashirika ya msalaba mwekundu katika mataifa husika.
Iwapo atafualu kupata nambari za simu , wahudumu wa shirika la msalaba mwekundu nchini Kenya wanapa nafasi ya kupiga simu mara moja kwa mwezi kwa angalau dakika mbili.
Kwa wale ambao wana wanafamilia ambao wana simu za kisasa kuna huduma ya WIFI katika maeneo maalum na kwenye ofisi za Kenya Redcross ambapo wanaunganishwa na kupiga simu kutumia WhatsApp au Facebook ,mfumo ambao ICRC na Kenya Redcross zinasema ni maarufu kwa kuwa wakimbizi hao wanaweza kuonana kwa njia ya video na wapendwa wao.

Kupitia mfumo wanapata muda mwingi wa kuzungumza kwa kuwa gharama yake ni ndogo.
Kwa wale ambao hawajafanikiwa kupata namba ya simu ,huendelea kuwasiliana kwa njia ya ujumbe maalum au barua.
Mary Muteti kutoka Kenya Red Cross eneo la Kakuma anasema wakimbizi hao wanapozungumza na wapendwa wao ,wanakuwa watulivu na kuweza kuishi kwa matumaini.

ICRC inasema mwaka jana katika kambi ya Kakuma na Daadab iliweza kufanikisha simu
123, 767 zinazotumia WIFI na kusambaza ujumbe 4,041