Katika hatua ya kukabiliana na hatari ya milipuko ya moto vijijini kutokana na wananchi kuhifadhi mafuta ndani ya nyumba zao, Wakala wa Umeme Vijijini (REA) imezindua mpango wa kuanzisha vituo vidogo vya mafuta vijijini.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Jones Olotu amesema wananchi na kampuni binafsi wanaweza kupata mkopo wa hadi shilingi milioni 133 kuanzisha biashara salama ya uuzaji wa mafuta, ikizingatia viwango vinavyokubalika kisheria.
Mpango huu unalenga kuhakikisha usalama wa maisha na mali, huku nishati ikipatikana kwa urahisi vijijini na kupunguza majanga yanayoweza kuepukika.
✍ Mwandishi Wetu
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates