Benki ya Equity Tanzania imeahidi kuendelea kuwekeza katika teknolojia za kidigitali na kuongeza elimu ya fedha kwa wananchi, ikiwa ni juhudi za kukuza ujumuishaji wa kifedha nchini.
Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Isabella Maganga, amesema benki inaendelea kuimarisha ubunifu ili kuhakikisha wateja wanapata huduma bora na nafuu.
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates