Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa juma la vijana kitaifa linalotarajiwa kufanyika Mbeya Oktoba 10 mwaka huu, kuelekea kilele cha Mwenge wa Uhuru Oktoba 14 na maadhimisho ya miaka 26 ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Ridhiwani Kikwete, amesema hayo jijini Mbeya mapema leo alipokuwa akizungumza na wanahabari.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *