Mkurugenzi wa Mazingira wa Wizara ya Nishati, Emilian Nyanda amesema Tanzania inaandaa mpango wa kuongeza matumizi ya nishati safi kama sehemu ya utekelezaji wa mpango wa kitaifa wa matumizi ya nishati safi ya kupikia, ambapo tangu kuanza kwake idadi ya kaya zinazotumia nishati hiyo imeongezeka.

Amesema hayo katika maonesho ya teknolojia mbalimbali za nishati yaliyokutanisha washiriki kutoka nchi zaidi ya 25, yakilenga kubadilishana uzoefu na kuhamasisha matumizi ya teknolojia rafiki kwa mazingira.

#AzamTVUpdates
✍Rebeca Mbembela
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *