Meli ya MV Mwanza imefanya safari ya pili ya majaribio leo, Oktoba 8, 2025, ikiwa imebeba abiria na mizigo kutoka jijini Mwanza kupitia Bandari ya Kemondo hadi Bandari ya Bukoba.
Safari hiyo ni hatua ya pili ya ukaguzi wa utayari kabla ya meli hiyo kuruhusiwa rasmi kuanza kutoa huduma za usafiri katika Ziwa Victoria.
#AzamTVUpdates
✍Warda John
Mhariri| John Mbalamwezi