Bruno Fernandes alijiunga na Manchester United mnamo 2020 kutoka Sporting

Chanzo cha picha, Getty Images

Nahodha wa Manchester United Bruno Fernandes ,31, hana mpango wa kuondoka klabu hiyo mwezi Januari licha ya Mreno huyo kumezewa mate na vilabu kadhaa ya Saudi Arabia.(Talksport)

Mlinzi wa kati wa United na timu ya England Harry Maguire ,32, ana imani ya kupewa mkataba mpya baada ya mkataba wake kukamilika mwisho wa msimu huu.(Sun).

Kiungo wa kati wa Manchester City Bernardo Silva,31, anajipanga kufunganya virago aondoke klabu hiyo mwisho wa msimu huu, hata hivyo kuna vilabu kadhaa vya Saudia na pia Benfica ya Ureno wote wanainyemelea saini yake. (Givemesports)

Chelsea wako tayari kupokea maombi ya kibiashara kuhusu mshambuliaji chipukizi Tyrique George ,19, mnamo mwezi Januari. (Footballinsider)

West Ham, Real Sociedad na Valencia japo kwa mkopo mwezi Januari. (Estadio Deportivo)

Klabu ya Orlando City ya ligi kuu ya soka Marekani inataka kumsajili mshambuliaji wa Tottenham Hotspur Richarlison,28 wakati wa uhamisho wa majira ya joto mwaka 2026 na tayari washapiga gumzo na mshambuliaji huyo wa Brazil. (Fabrizio Romano)

Mshambuliaji kinara wa Juventus Dusan Vlahovic ,25, ana hamu ya kucheza katika ligi kuu ya England mwaka 2026 huku raia huyo wa Serbia akivutiwa sana na Chelsea na Tottenham.(TBR Football)

Manchester United wameitangulia Liverpool katika azimio la kumsajili mshambuliaji wa Bounemouth na Ghana Antoine Semenyo(Caught offside)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *