
Chanzo cha picha, Donwilson Odhiambo / Getty Images
-
- Author, Luis Barrucho and Tessa Wong
- Nafasi, BBC World Service
Kuanzia Morocco hadi Madagascar, Paraguay hadi Peru, maandamano yanayoongozwa na vijana yanaenea duniani kote huku vijana wa Gen Z wa umri wa miaka 13 hadi 28 wakielekeza kuchanganyikiwa kwao na serikali na kudai mabadiliko.
Vijana wa kizazi kipya (Gen Z) wanazidi kushika usukani wa harakati za kijamii na kisiasa kote duniani, na linalofanana zaidi ni chachu inayopatikana katika mitandao ya kijamii.
Lakini wataalam wameonya kuwa huenda ari yao ikawatumbukia nyongo siku za usoni.
Maandamano yakilalamikia uhaba wa maji na umeme yalipelekea kuvunjiliwa mbali kwa serikali ya Madagascar. Maandamano ya kupinga ufisadi na upendeleo yanasababisha kujiuzulu kwa waziri mkuu nchini Nepal. Nao Gen Z wa Kenya waliingia mitaani na mitandao ya kijamii kudai uwajibikaji wa serikali na mageuzi.

Chanzo cha picha, Klebher Vasquez / Anadolu via Getty Images
Huko Peru, vijana wakiwa bega kwa bega na madereva wa basi na teksi waliandamana hadi bungeni, wakilalamikia kashfa za ufisadi na hali mbaya ya usalama.
Nchini Indonesia, wafanyakazi wa ajira zisizo rasmi walipinga vikali mipango ya kupunguza huduma za ustawi wa jamii.
Nchini Morocco, maandamano makubwa zaidi dhidi ya serikali kwa miaka mingi yalishuhudiwa. Waandamanaji walitaka huduma bora za afya na elimu, huku wakikosoa matumizi ya mabilioni kwenye ujenzi wa viwanja vya Kombe la Dunia.

Chanzo cha picha, Abu Adem Muhammed / Anadolu via Getty Images
Mitandao ya kijamii kama chombo cha mabadiliko
Katika maandamano haya yote, mitandao ya kijamii imetumika kama jukwaa la kusimulia hadithi, kuonyesha mshikamano, kupanga mikakati, na kushirikiana maarifa kutoka nchi mbalimbali.
Kwa mujibu wa Janjira Sombatpoonsiri kutoka Taasisi ya Ujerumani ya Utafiti wa Kimataifa, haya ni sehemu ya “wimbi la miaka 15 la maandamano yanayoongozwa na vijana, likichochewa na uunganishwaji wa kidijitali.”
Wimbi hili linajumuisha matukio kama vile:
- Arab Spring (2010–2011)
- Occupy Wall Street (2011)
- Indignados Movement nchini Hispania (2011–2012)
- Maandamano ya kudai demokrasia nchini Thailand (2020–21)
- Sri Lanka (2022) na Bangladesh (2024)

Chanzo cha picha, Akila Jayawardana / NurPhoto via Getty Images
Ufisadi unapoonekana machoni
Athena Charanne Presto, mwanasosholojia kutoka Chuo Kikuu cha Kitaifa cha Australia, anasema kuwa mitandao ya kijamii imegeuza taarifa za kisiasa kuwa ushahidi unaoonekana.
“Wakati ufisadi unapotajwa kwenye ripoti au kesi za kisheria, huwa ni jambo la mbali. Lakini watu wakiona kupitia simu zao kwenye picha za majumba ya kifahari, magari ya kifahari, na maisha ya anasa ufisadi unakuwa halisi.”
Mwezi Septemba nchini Nepal, picha ya mtoto wa mwanasiasa akipiga picha mbele ya mti wa Krismasi uliotengenezwa kwa masanduku ya bidhaa ghali ziliibua hasira kubwa.
Tendo hilo lilionekana kama dhihaka kwa maisha magumu ya watu wa kawaida.
Mambo kama hayo pia yalijitokeza Ufilipino, ambapo vijana walihusisha maisha ya kifahari ya wanasiasa na ufisadi kwenye miradi ya kuzuia mafuriko, ambayo watu wengi hufa kutokana nayo.

Chanzo cha picha, Prabin Ranabhat / AFP via Getty Images
“Hivi ndivyo [Gen Zs] walikua navyo – hivi ndivyo wanavyowasiliana,” Bw Feldstein anasema.
“Jinsi kizazi hiki kinavyojipanga ni dhihirisho la asili la hilo.”
Picha na machapisho husafiri zaidi na kwa kasi zaidi kuliko hapo awali, na kuongeza hasira na mshikamano.
Athena Charanne Presto, mwanasosholojia katika Chuo Kikuu cha Kitaifa cha Australia, anasema: “Mitandao ya kijamii imegeuza kile ambacho kinaweza kuonekana kama chapisho la maisha kuwa ushahidi wa kisiasa na, mara nyingi, kilio cha kuhamasisha.
“Rushwa mara nyingi huhisi kuwa ni kitu cha kufikirika inapozungumzwa katika ripoti au kesi za kisheria – lakini watu wanapoiona kwenye vyombo vyao, rushwa inakuwa halisi.
“Sasa katika mfumo wa majumba ya kifahari, magari ya michezo, mifuko ya ununuzi wa kifahari, umbali kati ya fursa za wasomi na ugumu wa kila siku basi inakuwa tusi la kibinafsi, ambapo wazo la kimuundo na dhahania la ufisadi linaporomoka katika sehemu zinazoweza kueleweka.”

Chanzo cha picha, Instagram / sgtthb
Hivi ndivyo ilivyokuwa Septemba hii nchini Nepal – ambapo maandamano yalichochewa na picha ya Instagram ya mtoto wa mwanasiasa akiwa amepiga kando ya mti wa Krismasi uliotengenezwa kwa masanduku ya nembo ya kifahari – lakini pia nchini Ufilipino.
“Kama Nepal, hii iliwagusa vijana nchini Ufilipino kwa sababu ilionyesha jambo ambalo tayari walijua – kwamba wasomi wa kisiasa wanaishi kupita kiasi,” Bi Presto anasema.
“Na kwa upande wa Ufilipino, unyanyasaji huu unachangiwa moja kwa moja na ukweli kwamba wanasiasa wanaiba kutoka kwa miradi ya kudhibiti mafuriko ambapo Wafilipino wanazidi kuzama.”

Chanzo cha picha, Delphia Ip / NurPhoto via Getty Images
Mitandao ya kijamii pia imewezesha wanaharakati kushirikiana mikakati ya maandamano kutoka nchi moja hadi nyingine.
Mfano ni #MilkTeaAlliance, mtandao wa wanaharakati wa kidemokrasia wa Asia uliozaliwa kutoka maandamano ya Hong Kong mwaka 2019.
Wanaharakati nchini Thailand walitumia mbinu ya “kuwa maji” (be water) — kutangaza maandamano mahali fulani kisha kubadilisha dakika za mwisho kupitia Telegram, wakihadaa polisi na kuepuka kukamatwa.
“Mbinu hii ilisaidia raia kukwepa ufuatiliaji na kukamatwa,” Bi Sombatpoonsiri anasema.
Athari mbili za mitandao ya kijamii

Chanzo cha picha, Anusak Laowilas / NurPhoto via Getty Images
Kadiri maandamano ya mtandaoni yanavyoenea, tawala za kidikteta zimeanza kujibu kwa kuzuia uhuru wa vyombo vya habari na kutumia nguvu.
Lakini wataalamu wanaonya kuwa hatua hizi mara nyingi huishia kuchochea maandamano zaidi hasa pale watu wanapoona picha za mateso au vifo vya waandamanaji moja kwa moja.
Mnamo 2024 nchini Bangladesh, serikali ya Awami League ilizima intaneti, ikakamata wakosoaji na kutumia risasi dhidi ya wanafunzi waliokuwa wakiandamana.
Lakini picha ya mwanafunzi Abu Sayed, aliyepigwa risasi na kuuawa na polisi, ilimfanya kuwa shujaa na kuchochea maandamano makubwa zaidi.
Mambo kama haya yamejiri pia katika Sri Lanka, Indonesia na Nepal ambapo vifo vya waandamanaji vilizidisha hasira, kuimarisha madai ya mabadiliko, na katika baadhi ya matukio, kuangusha serikali.

Chanzo cha picha, NurPhoto via Getty Images
Mitindo kama hiyo ilifanyika huko Sri Lanka, Indonesia na Nepal, ambapo mauaji ya waandamanaji yalichochea hasira, madai magumu na, wakati mwingine, kupindua serikali.
Ingawa mitandao ya kijamii inaimarisha vuguvugu la maandamano, hata hivyo, pia inawaweka kwenye mgawanyiko na ukandamizaji.
Kuandaa bila viongozi kunatoa “kubadilika na hali ya usawa”, Bi Sombatpoonsiri anasema, lakini anaamini kuwa kunaweza kuacha makundi katika hatari ya kujipenyeza, ghasia au ajenda zinazobadilika.
Uongozi usio rasmi katika maandamano unatoa nafasi ya usawa na uhuru, lakini pia huwa dhaifu mbele ya changamoto kama:
- Kupenyezwa kwa mawakala wa serikali,
- Kuegemea vurugu,
- Au kupoteza mwelekeo.

Chanzo cha picha, Anusak Laowilas / NurPhoto via Getty Images
Huko Thailand, harakati za mwaka 2020 zilikumbwa na mgawanyiko baada ya mitandao ya kijamii kujaa alama za ukomunisti na hashtag kama #RepublicOfThailand, jambo lililowakatisha tamaa washirika wengine wa harakati.
Na huko Nepal na Bangladesh, maandamano yaliyoratibiwa kiholela mara kwa mara yaliongezeka katika vurugu.
Wakati huo huo, utafiti unapendekeza serikali zinageuza zana za kidijitali dhidi ya wanaharakati.
“Tangu Majira ya Kiarabu, serikali zimeanzisha ufuatiliaji unaoendeshwa na AI, udhibiti mkali zaidi, na sheria kandamizi, na kuwalazimisha wanaharakati kufanya kazi chini ya hatari ya mara kwa mara,” Bi Sombatpoonsiri anasema.

Chanzo cha picha, Patrick Baz / AFP via Getty Images
Je, maandamano haya yana matokeo ya kudumu?
Wataalamu pia wanajadili athari za muda mrefu za maandamano yanayoongozwa na mitandao ya kijamii.
Utafiti wa Chuo Kikuu cha Harvard (2020) unaonyesha:
Miaka ya 1980–1990: Asilimia 65 ya harakati zisizo na silaha zilifanikiwa.
Miaka ya 2010–2019: Idadi hiyo ilishuka hadi asilimia 34.
Sombatpoonsiri anasema: “Hata kama maandamano yanang’oa serikali, si rahisi kuleta mabadiliko ya kweli.
Maandamano yanaweza kubadilika kuwa vita vya wenyewe kwa wenyewe kama ilivyotokea Syria, Myanmar na Yemen.
Au viongozi wa zamani wa kiimla wanaweza kurudi na kuimarika tena kama ilivyotokea Misri, Tunisia na Serbia.”
“Hata harakati za watu wengi zinapoleta mabadiliko katika serikali au tawala, mabadiliko ya muda mrefu hayana uhakika,” Bi Sombatpoonsiri anasema.
“Maandamano yanaweza kuingia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe, kama vile Syria, Myanmar, na Yemen, na kusababisha makundi yanayohasimiana kugombea madaraka, au watawala wa kiimla wanaweza kurejea na kuunganisha ushawishi wao, kama vile Misri, Tunisia na Serbia, kwani mageuzi yanashindwa kubomoa miundombinu iliyoimarishwa ya serikali zilizotangulia.”
Zaidi ya hashtag

Chanzo cha picha, FITA / AFP via Getty Images
Steven Feldstein anasisitiza kuwa mitandao ya kijamii haiwezi peke yake kuleta mabadiliko ya muda mrefu:
“Unategemea hasira, algorithms, na hashtagi. Lakini mabadiliko ya kweli yanahitaji harakati zinazojengwa kwa ushirikiano wa kweli si tu mtandaoni bali pia ana kwa ana.”
Sombatpoonsiri anaongeza: “Tunahitaji mikakati ya mseto kwa kuunganisha harakati za mtandaoni na zile za jadi kama migomo, maandamano ya wazi, na mikutano ya hadhara.
Muhimu zaidi, ni kuwa na ushirikiano mpana kati ya mashirika ya kiraia, vyama vya siasa, taasisi rasmi na wanaharakati wa kidijitali.”
Imetafsiriwa na Mariam Mjahid