
Guterres amesema mateka wote lazima waachiliwe huru kwa njia ya heshima, na usitishaji wa vita wa kudumu lazima ufanyike.
Amezipongeza Marekani, Qatar, Misri na Uturuki ambazo zimesaidia kufanikisha makubaliano hayo katika mazungumzo yaliyofanyika Sharm el-Sheikh, Misri.
Umoja wa Ulaya wapongeza
Wakati huo huo, Umoja wa Ulaya umesema kufikiwa kwa makubaliano hayo ni mafanikio makubwa.
Mkuu wa Sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya, Kaja Kallas amesema Alhamisi kuwa hatua ya Israel na Hamas kufikia makubaliano hayo ni mafanikio makubwa ya kidiplomasia na nafasi ya kweli ya kuvimaliza vita na kuwaachilia mateka wote.
Kallas amesema Umoja wa Ulaya utafanya kila kila uwezavyo kuhakikisha makubaliano hayo yanatekelezwa.