
Hoja mbili zilizowasilishwa na wabunge wa siasa kali za mrengo wa kulia wanaojulikana kama Wazalendo wa Ulaya, na wabunge wa vyama vya mrengo wa kushoto, zilishindwa kupata angalau kura 360, zinazowakilisha robo tatu ya kura zote zilizopigwa.
Hoja ya wanasiasa wa mrengo mkali wa kulia iliungwa mkono na wabunge 179, huku 378 wakipiga kura kupinga na 37 walijizuia.
Alisalimika tena kura ya Julai
Hoja ya wanasiasa wa mrengo wa kushoto iliungwa mkono na wabunge 133, huku 383 wakipiga kura kupinga na 78 walijizuia.
Mnamo mwezi Julai, Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya na timu yake walikabiliwa pia na kura nyingine ya kutokuwa na imani nao.
Von der Leyen amesalimika kutokana na migawanyiko ya kisiasa kati ya wabunge wa Umoja wa Ulaya, lakini kura hizo zinaonyesha ukosoaji unaoongezeka kuhusu sera zake.