
Katibu Mkuu wa Taasisi ya Sweden inayoandaa Tuzo za Nobel, Mats Malm amesema Alhamisi kuwa Krasznahorkai ametunukiwa tuzo hiyo kutokana na juhudi zake za kipekee na zenye maono mapana, ambazo hata katikati ya hofu na machafuko ya dunia, zinaonyesha tena nguvu na uzuri wa sanaa.
Kazi zake kadhaa ikiwemo Satantango na The Melancholy of Resistance, zilibadilishwa na kuwa filamu na mtengeneza filamu wa Hungary, Béla Tarr.
Tuzo inaambatana na fedha
Tuzo hiyo inaambatana na dola milioni 1.2 za Kimarekani.
Tuzo ya Nobel ya Fasihi kwa mwaka uliopita ilikwenda kwa mwandishi wa Korea Kusini Han Kang, ambaye alikuwa raia wa kwanza wa Korea Kusini na mwanamke wa 18 kushinda tuzo hiyo.
Mwanamke wa kwanza alikuwa mwandishi wa Sweden, Selma Lagerlof aliyeshinda tuzo hiyo mwaka 1909.