Akizungumza Alhamisi mjini Brussels, Ubelgiji, katika Jukwaa la Global Gateway, Tshisekedi amemsihi Kagame washirikiane kwa pamoja katika kuleta amani.

“Ndiyo maana nakuomba kupitia jukwaa hili, na huku ulimwengu mzima ukishuhudia, kukuomba Mheshimiwa Rais, ili tulete amani,” alisisitiza Tshisekedi.

Tshisekedi amesema wito huo unahusisha Kagame kuliamuru Kundi la M23 kusitisha mapigano ambayo tayari yamesababisha vifo vingi.

Kagame hajazungumza wazi

Katika hotuba yake, Rais Kagame hakuuzungumzia moja kwa moja mgogoro huo.

Hata hivyo, alirejelea kwa kifupi kauli ya awali ya Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa aliyesema anahisi “msukumo wa kutaka amani” alipowaona pamoja viongozi wa Rwanda na Kongo.

Hata hivyo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, Olivier Nduhungirehe amesema mtu pekee ambaye anaweza kuvimaliza vita vya Kongo ni Rais Tshisekedi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *