Rais Felix Tshisekedi ametoa wito kwa mwenzake wa Rwanda Paul Kagame “kukumbatia amani” na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Tshisekedi, 62, alitoa wito huo katika mkutano jijini Brussels, Ubelgiji baada ya Kagame kuhutubia kongamano hilo.

“Natoa wito na mkutano huu ni mashahidi, na dunia nzima, kutafuta amani, Bwana Rais, ili tuweze kuwa na amani,” Tshisekedi alisema.

Mashariki mwa DRC, eneo linalopakana na Rwanda na lina raslimali nyingi za asili, limekumbwa na vurugu kwa zaidi ya miongo mitatu. DRC inadai Rwanda inaunga mkono kundi la waasi la M23, ambalo linaendeleza harakati zake mashariki mwa DRC, lakini Rwanda inakanusha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *