Beki wa Crystal Palace na England Marc Guehi

Chanzo cha picha, Getty Images

Beki wa Crystal Palace na England Marc Guehi, 25, amempiku beki wa kati wa Liverpool na Ufaransa Ibrahima Konate, 26, kama mchezaji anayepigiwa upatu kusajiliwa bila malipo na klabu ya Real Madrid msimu ujao. (Fichajes – kwa Kihispania)

Liverpool wanavutiwa na beki wa kati wa Bayern Munich na Ufaransa Dayot Upamecano, 26, pamoja na Guehi wa Crystal Palace. (Florian Plettenberg)

Tottenham ni miongoni mwa klabu zinazomfuatilia kwa karibu mshambuliaji wa Brentford Mjerumani Kevin Schade, 23. (Sky Germany via Sky Sports)

Juventus wanamtaka mlinda lango wa AC Milan Mfaransa Mike Maignan, 30, ambaye mkataba wake unamalizika msimu ujao. Kipi huyo pia anawaniwa na Chelsea na Bayern Munich. (Gazzetta dello Sport – kwa Kiitaliano)

Inter Miami wanapania kuunda tena safu ya mashambulizi itakayowakutanisha washambuliaji mashuhuri wa zamani wa klabu ya Barcelona kama vile Mrazil Neymar, 33, na Muargentina Lionel Messi na Muruaguay Luis Suarez. (Mail)

Kiungo mshambuliaji wa Levante na Cameroon Etta Eyong, 21, angependelea kujiunga na Barcelona badala ya Manchester United. (Sport – kwa Kihispania)

Bayern Munich wanavutiwa na Murillo wa Nottingham Forest, 23, lakini watahitaji kuwauza wachezaji kwanza ili kufadhili uhamisho wa beki huyo wa kati wa Brazil. (Bild – kwa Kijerumani)

Mike Maignan

Chanzo cha picha, Getty Images

Liverpool, Chelsea na Manchester United ni miongoni mwa vilabu vinavyowania dau la euro 60m (£52.2m) la kumsajili beki wa RB Leipzig Mfaransa Castello Lukeba, 22.

Tottenham wanamtaka winga wa Nigeria Sani Suleiman mwenye umri wa miaka 19 baada ya kutuma maskauti kumtazama akiwa kwenye harakati za kuichezea AS Trencin ya Slovakia. (Team talk)

Kiungo wa kimataifa wa England na klabu ya Crystal Palace Adam Wharton, 21, anaridhika kuwa Selhurst Park na hana mpango wa kuondoka mwezi Januari licha ya Liverpool, Manchester City na Real Madrid kuonyesha nia ya kutaka kumsajili. (Football Insider)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *