
Waziri Mkuu wa Ufaransa Sébastien Lecornu ameelezea kushangazwa kwake na hatua ya Rais Emmanuel Macron ya kumteua tena kuwa waziri mkuu wa taifa hilo baada ya kutangaza kujiuzulu kwake mwanzoni mwa wiki.
Lecornu, mshirika wa karibu wa Macron, aliyeteuliwa kwa mara ya kwanza kushika nafasi hiyo wiki nne zilizopita alijiuzulu siku ya Jumatatu kutokana na mzozo wa kisiasa unaoendelea kuikabili nchi hiyo.
Kurejea kwake kulithibitishwa jana Ijumaa baada ya Macron kumpa tena jukumu la kuwa na mazungumzo na upinzani kupata njia ya muafaka ya kusonga mbele baada ya miezi kadhaa ya msukosuko huo wa kiasia uliosababishwa na sheria mpya ya uzeeni na suala la kuongezewa kwa bajeti.
Chini ya katiba ya Ufaransa bajeti mpya ya serikali kwa mwaka ujao inapaswa kuwasilishwa bungeni na Waziri Mkuu ifikapo siku ya Jumatatu.