
Msemaji huyo amesema kama sehemu ya mipango ya matibabu Biden anapokea pia matibabu ya homoni.
Joe Biden ambaye atafikisha miaka 83 mwezi ujao, mwezi Septemba alifanyiwa upasuaji kuondoa seli za saratani katika ngozi yake.
Mwezi Mei kiongozi huyo wa zamani aliyetokea chama cha Democratic aligundulika kuwa na aina hiyo kali ya saratani ya tezi dume ambayo imesambaa hadi kwenye mifupa yake.