
Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester United wanamfuatilia kwa karibu Adam Wharton, Reds hawatamchukulia Thomas Tuchel kama mbadala wa Ruben Amorim, Vinicius Junior kumfungulia njia Erling Haaland huko Real Madrid.
Adam Wharton, 21, analengwa na Manchester United. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza anapendwa sana Old Trafford na klabu hiyo inaweza kutoa ofa ya pauni milioni 60 kumnunua kiungo huyo wa Crystal Palace. (Mirror)
Wakati huo huo, United haitamchukulia meneja wa England Thomas Tuchel kama mbadala anayeweza kushika nafasi hiyo iwapo watamtimua Ruben Amorim. (Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images
Bayern Munich wamedhamiria kuongeza mkataba wa beki Dayot Upamecano, 26, huku Liverpool ikivutiwa naye, licha ya klabu hiyo ya Ujerumani kushindwa kukubaliana nyongeza ya ofa ya mlinzi huyo wa kati ambaye anaweza kuondoka bila malipo mwezi Juni 2026. (Florian Plettenberg)

Chanzo cha picha, Getty Images
Real Madrid wanapanga kumuuza mshambuliaji Vinicius Junior, 25, kwa ada itakayoweka rekodi katika jitihada za kufadhili usajili wa mshambuliaji wa Manchester City Erling Haaland, 25. (CaughtOffside)
Klabu ya Uturuki Galatasaray inaongoza katika kinyang’anyiro cha kumsajili beki wa United mwenye umri wa miaka 26 Tyrell Malacia. (Star)

Chanzo cha picha, Getty Images
Nottingham Forest wameonyesha nia kabisa kwa Rafael Benitez kama mbadala wa Ange Postecoglou iwapo wataamua kuachana na meneja huyo wa Australia. (Football Insider)
Manchester United wanakabiliwa na Tottenham Hotspur kumnunua kiungo wa kati wa Sporting Morten Hjulmand mwenye umri wa miaka 26. (Fichajes – in Spanish)

Chanzo cha picha, Getty Images
Crystal Palace wamemtambua beki wa West Ham United Max Kilman, 28, kama mbadala wa Marc Guehi iwapo beki huyo wa kati wa England ataondoka katika dirisha la uhamisho la Januari. (Football Insider)
Beki wa Uingereza na Manchester United Harry Maguire, 32, atakataa ofa yoyote ya pesa nyingi kutoka Saudi Arabia ikiwa klabu hiyo itampa mkataba mpya. (Star)

Chanzo cha picha, Getty Images
Kiungo wa kati wa Chelsea Enzo Fernandez, 24, anafuatiliwa na Real Madrid lakini The Blues wanadai dau la angalau £120m kwa mshindi huyo wa Kombe la Dunia. (Fichajes – in Spanish)
Mshambulizi wa Manchester United Joshua Zirkzee, 24, ameibuka kama mchezaji anayelengwa Januari na klabu ya Serie A ya Roma. (Gazetta dello Sport – in Italian)
Imefasiriwa na Asha Juma