
Umoja wa Ulaya umesema utaratibu huo ni kwa ajili ya kudhibiti usalama mipakani na kufuatilia mienendo ya wageni wasio raia wa Umoja wa Ulaya.
Halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya mjini Brussels, imesema mfumo huo wa kibayometriki utanasa data za alama za vidole na picha za wasafiri.
Ujerumani mfumo mpya umeanza kutumika kwenye kiwanja gani cha ndege?
Nchini Ujerumani, mfumo huo mpya unaojulikana kama (EES) umeanza kutumika katika uwanja wa ndege wa Düsseldorf, halafu baadae vitafuata viwanja vya ndege vya Frankfurt na Munich.